Jumanne 18 Agosti 2026 - 11:38
Tokeni katika kile mnachokiita “mazungumzo” na simameni pamoja na watu wenu

Hawza/ Baraza la Wanazuoni wa Beirut limetangaza kwamba: Adui wa Kizayuni kusini mwa Lebanon ametenda mauaji ya kutisha dhidi ya raia wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto, ili kuongeza kwenye rekodi yake ya uhalifu na tabia yake ya uchokozi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Wanazuoni wa Beirut limetangaza katika taarifa kwamba: Adui wa Kizayuni kusini mwa Lebanon ametenda mauaji ya kutisha dhidi ya raia wasio na hatia, wakiwemo wanawake na watoto, ili kuongeza kwenye rekodi yake ya uhalifu na tabia yake ya uchokozi; tabia ambayo ni kuua, kuharibu na kuteketeza kila kinachohusiana na maisha, huku yote hayo yakitokea mbele ya macho na masikio ya viongozi wa Lebanon.

Taarifa hiyo iliendelea kusema: Sisi kama Baraza la Wanazuoni wa Beirut tunalaani kitendo hiki cha kihalifu na cha kinyama, na tunawataka viongozi hawa watoke katika kile wanachokiita “mazungumzo” na wasimame pamoja na wananchi wao wanaouawa, huku miji na vijiji vyao vikiharibiwa; ikiwa kwa kweli, kama wanavyodai, wana mamlaka ya kutekeleza matakwa yao ya kiutawala, basi waache ukimya wao mbele ya janga la kile kinachoendelea na wakiri kushindwa kwao pamoja na ahadi zao za zisizo za kweli! Je, wamewaletea watu usalama na kuwawezesha kurejea katika nyumba zao zilizoharibiwa? Na je, mauaji ya kila siku yamesitishwa, licha ya wao kumpa adui matakwa yote yanayoweza kufikiriwa na yasiyoweza kufikiriwa kwa upendeleo na bure, kiasi kwamba mwenendo huu umekuwa chanzo cha dhihaka na mshangao kwa taasisi nyingi za Kiarabu na za kigeni!

Taarifa hiyo iliongeza kuwa: Tunawabebesha viongozi jukumu la matokeo haya ya kusikitisha yaliyotokea; kutokana na msimamo wao wa kujifungia katika kuchagua mazungumzo ya moja kwa moja na adui, kujisalimisha kwao kwa woga mbele ya maagizo ya kigeni, na kuruhusu kwao aina zote za uingiliaji katika mambo yetu ya ndani. Hawakuilinda ardhi wala mamlaka ya nchi, bali hata kitendo cha muqawama walikichukulia kuwa ni uhalifu na wakazuia pia haki ya kujilinda!!

Mwishoni mwa taarifa hiyo imeelezwa kuwa: Tunaamini kwamba chaguo la muqawama ndiyo njia pekee ya kuikomboa ardhi, kulinda mamlaka ya nchi na kuhifadhi heshima ya kitaifa. Na viongozi hawa waliokata tamaa wajue kwamba damu ya watu wetu, ardhi yetu, miji na vijiji vyetu ni vitu pendwa na vyenye thamani kubwa sana; na kwamba watu wa muqawam ni watu wenye heshima na fahari, ambao hawakubali udhalili na unyonge, na historia yetu ni shahidi kenye madai haya.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha